Wednesday, July 24, 2013

Ferry - Tunavuka


Wananchi Wakipanda na Kushuka Vivuko Eneo la Ferry Dar es Salaam. Vivuko Hivi Vimerahisisha Mwenendo wa Watu katika Eneo hilo kati ya Magogoni na Kigamboni.

Sunday, May 3, 2009

Hakika Kilimanjaro ni Paa la Afrika

Mpiga picha wa tanzaniahalisi aliipata picha hii ya mlima mrefu Afrika, Mlima Kilimanjaro akiwa kwenye kipando cha Air Tanzania 'the wings of Kilimanjaro'. Mandhari hii haimithiliki na kuiona ni hivyo tu sio kuupanda mlima. jaribu Yote mawili.

Mapango ya Amboni


Hili ni eneo la mlango wa kuingilia Mapango ya Kale ya Amboni nje kidogo ya JIJI la Tanga. Ni sehemu usiyopaswa kuikosa ukiwa matemebezini au kikazi Tanga. Ila angalia huyo simba mlangoni, jioni huwa anaamka (nilihadhithiwa hivyo)

Daraja La Mkapa, Ufunguo wa Korido la Kusini


Daraja la Mkapa maeneo ya Ikwirir Rufiji. Daraja hili limekuwa chachu ya mawasiliano kwa mikoa ya Lindi na Mtwara na wilaya zake, ambao walitegemea MV Mapinduzi kwa miongo kadhaa.

Sherehe Ya Harusi ni Ya Jamii


Maandalizi ya harusi huko Masuguru, Wilaya ya Nanyumbu Karibu na Daraja la Umoja kati ya Tanzania na Msumbiji Mkoani Mtwara

Saturday, May 2, 2009

Bongo Bwana Hatuko Nyuma

Ghorofa ilivyokutwa na mpiga picha wa tanzaniahalisi maeneo ya Matiri huko Ruvuma wilaya ya Mbinga. Sio lazima Zege na nondo kulala kama popo